Categories
2 Wafalme

2 Wafalme Utangulizi

Utangulizi

Kwa kuwa kitabu cha 1 Wafalme na hiki cha 2 Wafalme ni historia moja inayoendelea, taarifa za msingi kwa ajili ya kitabu hiki cha 2 Wafalme ziko katika utangulizi wa 1 Wafalme.

Mwandishi

Mwandishi wa kitabu hiki hajulikani, lakini mapokeo ya Kiyahudi yanasema ni nabii Yeremia, au kikundi cha manabii.

Kusudi

Kuonyesha yale yatakayowakuta wale wanaokataa kumfanya Mungu kuwa kiongozi wao wa kweli.

Mahali

Katika nchi ya Israeli.

Tarehe

Hakuna uhakika ni wakati upi hiki kitabu kiliandikwa.

Wahusika Wakuu

Eliya, Elisha, mwanamke Mshunami, Naamani, Yezebeli, Yehu, Yoashi, Hezekia, Senakeribu, Isaya, Manase, Yosia, Yehoyakimu, Sedekia, na Nebukadneza.

Wazo Kuu

Kuanguka kwa falme zote mbili za Israeli na Yuda kulisababishwa na kutokutii maagizo ya Mungu, na kuishi maisha ya dhambi. Hali hii iliwasababisha kuwa mateka na kukaa utumwani, nayo miji yao ikaharibiwa, hii ikiwa ni hukumu kutoka kwa Mungu.

Mambo Muhimu

Kitabu hiki kinaandika majanga mawili makubwa yaliyosababisha kuanguka kwa Israeli na Yuda:

1. Kuharibiwa kwa mji mkuu wa Israeli, yaani Samaria, na taifa kuchukuliwa kwenda utumwani;

2. Kuharibiwa kwa Yerusalemu, na Yuda kupelekwa utumwani.

Mgawanyo

Eliya na Elisha (

1:1–8:15

)

Wafalme wa Israeli na wa Yuda (

8:16–17:6

)

Israeli wachukuliwa mateka kwenda Ashuru (

17:7–23:37

)

Kuanguka kwa Yerusalemu (

24:1–25:30

).

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *