Categories
1 Nyakati

1 Nyakati Utangulizi

Utangulizi

Jina hili la kitabu “Mambo ya Nyakati” linaweza likafuatiliwa hadi kwa Yerome ambaye alilitumia katika tafsiri ya Kilatini ya Neno la Mungu, yaani “Vulgate.” Jina la kitabu hiki katika Kiyunani, “Mambo Yaliyorukwa,” linaonyesha ile hali ya watafsiri wa Agano la Kale katika “Septuagint” kwamba mambo yaliyomo katika vitabu hivi kimsingi yalikuwa mambo ya nyongeza yaliyokuwa yameachwa na vitabu vya Samweli na Wafalme.

Vitabu vya 1 na 2 Mambo ya Nyakati viliandikwa kwa ajili ya watu waliorudi Israeli kutoka utumwani, baada ya kutekwa na kupelekwa Babeli, ili kuwakumbusha kwamba walikuwa wa ukoo wa ufalme wa Daudi, na kwamba wao walikuwa watu wateule wa Mungu.

Mwandishi

Mapokeo ya Kiyahudi husema ni Ezra.

Kusudi

Kuunganisha watu wa Mungu, kufuatilia ukoo wa Daudi, na kufundisha watu sala iliyo ya kweli ambayo ndiyo hitaji kubwa katika maisha ya mtu binafsi na taifa pia.

Mahali

Yerusalemu, na katika Hekalu.

Tarehe

Kama mwaka wa 430 K.K.

Wahusika Wakuu

Daudi na Solomoni.

Wazo Kuu

Kitabu cha 1 Mambo ya Nyakati kinaelezea kwa kifupi historia na koo za Waisraeli tangu Adamu hadi kifo cha Mfalme Sauli. Sehemu ya kitabu iliyobaki inaeleza habari za Mfalme Daudi.

Mambo Muhimu

Kuelezea historia ya vizazi vya Israeli, na habari kumhusu Mfalme Daudi na uhusiano wake na Mungu, na kuletwa kwa Sanduku la Agano huko Yerusalemu kama chanzo cha sala ya kweli.

Mgawanyo

ORODHA YA VIZAZI (

1:1–9:44

)

1. Orodha ya nasaba za mababa wa taifa

2. Makabila ya Israeli

3. Kurudi kutoka utumwa Babeli.

UTAWALA WA DAUDI (

10:1–29:30

)

1. Daudi afanyika mfalme juu ya Israeli yote

2. Daudi alirudisha Sanduku la

Bwana

Yerusalemu

3. Majeshi ya Daudi yajinufaisha

4. Daudi aandaa kwa ajili ya ujenzi wa Hekalu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *